Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na viongozi mbalimbali wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha JNICC) jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa na kushoto kwake ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt.Doto Biteko.


Wageni pamoja na Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.