Rais wa IPU, Spika Dkt.Tulia aongoza kikao ofisini kwake jijiini Geneva

GENEVA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewasili Ofisini kwake Geneva nchini Uswisi leo tarehe 15 Mei, 2024 na kuongoza kikao cha utangulizi cha maandalizi ya kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani kinachotarajiwa kufanyika tarehe 16 na 17 Mei, 2024 nchini humo.
Kikao hicho kinatarajiwa kuhusisha Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na Kijiographia, Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na Uongozi wa Majukwaa na Umoja kwa ujumla wake.
Aidha, Mkutano huo wa Maspika Duniani utakaofanyika mwaka 2025 utaangazia kuweka ajenda za kuchakata changamoto zinazoendelea kuikumba Dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news