Rais wa IPU, Spika Dkt.Tulia aongoza kikao muhimu jijini Geneva

GENEVA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi. 
Kikao hicho kilichohusisha Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na Kijiographia, Wawakilishi kutoka Kamati ya Uongozi, Viongozi wa Makundi ya Wanawake na Vijana pamoja ya Uongozi wa Umoja huo kimejadili kuhusu mapendekezo ya ajenda za Mkutano huo wa Maspika unaotarajiwa kufanyika mwakani na kuona namna changamoto za sasa zinazoikumba Dunia zinavyoweza kuwa sehemu ya ajenda za Mkutano huo.
Baadhi ya changamoto zinazotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi, ukame na njaa hususani Sub Saharan Afrika, machafuko ya amani na vita zinazoendelea katika baadhi ya mataifa Duniani, usawa wa kijinsia na kujenga Jumuiya jumuishi na za ushilikishwaji. 

Aidha, mjadala wa demokrasia na matumizi ya akili bandia na matokeo yake nayo ni sehemu ya ajenda zinazotarajiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news