Rais wa IPU, Spika Dkt.Tulia atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Austria

VIENNA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 19 Mei, 2024 amewasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Austria na kupokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Naimi S. H. Aziz, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna.
Dkt. Tulia yupo Vienna nchini Austria, ambapo anatarajia kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Nyuklia (ICONS-2024) utakaofanyika kuanzia kesho tarehe 20-24 Mei, 2024 akiwakilisha IPU kwenye Mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news