TANGA-Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mheshimiwa Balozi Dkt.Batilda Salha Burian leo Mei 30,2024 ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maadhimisho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ambako amepata maelezo kuhusu majukumu na mchango wa TEA katika kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia.Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda Burian akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt. Erasmus F. Kipesha alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
Mheshimiwa Balozi Dkt.Burian ameipongeza TEA kwa kazi za uboreshaji miundombinu ya Elimu mkoani Tanga,ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 kuna miradi takribani sita inayotekelezwa kupitia ufadhili wa TEA katika halmashauri za Wilaya ya Korogwe, Mkinga, Tanga Jiji, Muheza na Handeni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt.Erasmus F. Kipesha akitoa maelezo kuhusu majukumu ya TEA kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda Burian alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt.Erasmus F. Kipesha (kushoto) akimsikiliza mdau katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga. Katikati ni Mwafatma Mohamed ambaye ni Kaimu Meneja Miradi kutoka TEA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt. Erasmus F. Kipesha akitoa zawadi maalum kwa Dkt.Joseph Sungau katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
Katika banda la TEA, mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga alipokelewa na kupewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha ambapo alimueleza kuhusu Mfuko wa Elimu wa Taifa wenye jukuku la kisheria la kukusanya rasilimali fedha na vifaa kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jitihada za Serikali za kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa.
Baadhi ya wadau wakiuliza maswali kwenye banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
TEA imekuwa miongoni mwa taasisi zilizoshiriki maonesho na maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza tarehe 25 hadi 31 Mei 2024 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal ya jijini Tanga ambapo mamia ya wananchi wamekuwa wakihudhuria katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupata elimu katika Sekta ya Elimu.
Bi.Mwanaasha Sendega kutoka COSOTA (kulia) akipatiwa elimu kwenye banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga. Kushoto ni Mwafatma Mohamed ambaye ni Kaimu Meneja Miradi kutoka TEA na katikati ni Afisa Uhusiano wa TEA, Eliafile Solla.
Dkt. Joseph Sungau kutoka Chuo Kikuu Mzumbe akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Dkt. Erasmus F. Kipesha akipatiwa huduma kwenye banda la Benki ya NMB, alipotembelea banda hilo katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga.
Maonesho hayo ambayo yamendaliwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yamehusisha taasisi mbalimbali za masuala ya elimu na mafunzo ambapo yameongozwa na kauli mbiu ya "Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi Shindani".