Serikali imeendelea kujipanga kukabiliana na magonjwa ya milipuko

DODOMA-Serikali ilikabiriana na maporomoko yaliyotokea Hanang Mkoani Manyara ambapo Wizara ya Afya iliratibu utoaji wa huduma za Afya na udhibiti wa athari za kiafya kwa kupeleka jumla ya wataalam 266 wenye taaluma mbalimbali ili kutoa huduma za Afya kwa waathirika.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni Mei 13, 2024 akiwa anawasilisha hotuba yake ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2024/25 akielezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika utoaji wa huduma za Kinga nchini.

"Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilieleka bidhaa za afya zenye thamani ya jumla Shilingi Bilioni 652,902,003.06 kwa ajili ya matibabu kwa majeruhi 139 waliolazwa katika vituo vya kutolea huduma,"amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema katika kuimarisha na kusimamia huduma za dharura na ajali, Wizara imekamilisha usimikaji wa vifaa vya EMD katika Hospitali Tano ambazo zilikuwa bado hazijapata vifaa vyote kupitia MSD, ikiwemo Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Kigoma, Lindi, Kagera, Katavi na Hospitali ya Lugalo.

"Pia, Wizara imeendelea na usambazaji wa magari ya kubebea wagonjwa 603 yaliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Halmashauri, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Kanda, Maalum na Taifa, lengo likiwa ni kuimarisha huduma za dharura, ajali na rufaa nchini,"amesema Waziri Ummy.

Amesema, ili kuhakikisha idara za dharura zilizojengwa katika Hospitali za ngazi zote zinaendeshwa na watoa huduma wenye ujuzi na weledi, Wizara kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa mafunzo kwa wataalam wa idara za dharura na ICU.

"Kwa Mwaka 2023/24, Wizara imetoa mafunzo kwa jumla ya watoa huduma 1,230 hivyo kufikisha jumla ya watoa huduma 5,385 waliopata mafunzo katika ngazi za Halmashauri, Mikoa, Kanda na Taifa,"amesema Waziri Ummy.

Amesema, kufuatia mvua juu ya wastani zinazoendelea kunyesha nchini, baadhi ya maeneo yalikumbwa na mafuriko yaliyosababisha athari nyingi ikiwemo athari za kiafya.

"Wizara kwa kushirikiana na timu za wataalam wa Mikoa ya Lindi, Pwani na Morogoro imeendelea kutekeleza afua za kinga na tiba za athari za kiafya zilizojitokeza," amesema Waziri Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news