Serikali kuja kisasa mikopo ya asilimia 10 nchini

DODOMA-Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema, Serikali imefanya maandalizi makubwa katika usimami wa mikopo ya asilimia 10.

Amesema, Serikali imeamua kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi wa mikopo hiyo kwa ngazi ya wizara, na kamati ya usimamizi wa mikopo hiyo katikati ngazi ya mikoa, Halmashauri na kata.
Mhe. Katimba amesema hayo leo Mei 16,2024 bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu.

Ni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Christina Christipher Mnzava aliyetaka kujua Serikali imejipanga vipi katika usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 pindi itakapoanza kutolewa tena kuanzia Julai 1, mwaka huu.

“Timu iliundwa kufanya mapitio na kuhakikisha unatengenezwa utaratibu bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha mikopo hii inatoka na inaenda kuwanufaisha walengwa na tayari katika Muundo wa usimamizi wa mikopo hii kutaanzishwa Kitengo cha usimamizi wa Mikopo hii katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI na kamati za usimamzizi wa Mikopo hii katika ngazi ya Mikoa, Kalmashauri na Kata,” amesema Mhe. Katimba.

Amesma,mikopo hii ya asilimia kumi inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashuri ilisitishwa kutokana na maelekezo ya serikali ya kuangalia upya utaratibu na changamoto zilizokuwepo hapo awali katika utoaji wa mikopo hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news