Serikali, sekta binafsi mguu sawa utekelezaji miradi

DODOMA-Wizara ya Ujenzi imeanza utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia (PPP) katika kutekeleza miradi ya miundombinu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25 bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024

Amesema,ni katika kuipunguzia Serikali gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya miundombinu hasa barabara na madaraja ambayo Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha.

“Lengo la kutumia utaratibu huu ni kujenga miundombinu na kuitekeleza kwa wakati.”

Aliitaja iradi inayotekelezwa kwa utaratibu huo kuwa ujenzi wa barabara ya Kibaha-Chalinze-Morogoro-Dodoma (Expressway) yenye urefu wa kilometa 423.8 kwa mfumo wa kulipia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news