Serikali yaanisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo nchini

DODOMA-Waziri wa Madini, Mhe.Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.
Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Mei 9, 2024 wakati akijibu swali la Mhe. Dkt. Christine Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.

Ameongeza kwamba, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo

Kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.

“Mhe. Spika maeneo mengine ni utoaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo; kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija; huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),” amesema Waziri Mavunde.

Vilevile, amesema kuwa, mpango mwingine ni kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji; na fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news