Serikali yaipongeza Sanku kwa urutubishaji wa vyakula nchini

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama amesema, mahitaji ya virutubishi vya chakula ni ajenda kubwa ambayo itachochea katika kuongeza ajira kwa wakulima nchini na kuwa na uhakika na virutubishi tunavyovitumia hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watendaji mbalimbali aliopotembelea Kiwanda cha Sanku (Sanku Project Healthy Children Ltd) kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Waziri amesema hayo Mei 25,2024 alipotemebelea na kukagua kiwanda cha Sanku (Sanku Project Healthy Children Ltd) kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho cha uchanganyaji wa virutubishi kwenye unga wa mahindi na ngano kwa bei nafuu.
Bw. Nyangwaka Ndili kutoka Jukwaa la Wasindikaji akieleza jambo Mbele ya Waziri wa Nchi alipotembelea na kufanya kikao na watendaji wa Kiwanda cha Sanku Kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam.

"Naomba muendeele kufanya ufuatiliaji wa karibu katika kutoa elimu ili kuondoa matatizo mengine ya udumavu, utapiamlo na shida ya kupungukiwa vitamini A kwa akinamama wajawazito."
Mhandisi Joseph Mtwangi akieleza jambo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,Mhe. Jensita Mhgama juu utendaji kazi wa vifaa mbalimbali katika Kiwanda cha Sanku.
Meneja Mwandamizi wa Sanku, Bw. Gwao Omari Gwao katika matukio tofauti akizungumza na Waziri wa Nchi wakati alipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Kiwanda cha Sanku.

“Hii kazi ni kazi yenye manufaa makubwa na itaweza kutusaidia sana kama nchi tuweze kusonga mbele na kusaidia kuitangaza nchi kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha kuchanganya virutubishi,” alisema Waziri Mhagama.
Meneja Mwandamizi wa Sanku Bw. Gwao Omari Gwao katika matukio tofauti akizungumza na Waziri wa Nchi wakati alipotembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika Katika kiwanda cha Sanku.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Sanku Bw. Gwao Omari Gwao amesema kampuni yao inasaidia wafanyabishara wadogo na wakati kufanya urutubishaji ambazo zimefunguliwa katika Mikoa 26 Tanzania Bara na katika Halmashauri 142 Tanzania Bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news