Serikali yaunda Kamati ya Uchambuzi viwango vya Pensheni

DODOMA-Serikali imesema kuwa, imeunda kamati ya kukusanya na kuchambua maoni na mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni ili kuwezesha maandalizi ya rasimu ya Waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu nyongeza ya pensheni kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina.
Hayo yameelezwa bungeni leo Mei 7,2024 jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo, aliyetaka kufahamu lini Serikali itawaongezea pesheni wastaafu wanaolipwa shilingi 100,000 kwa mwezi na Hazina.

Alisema kuwa Kazi ya uchambuzi wa maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni inatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni 2024.

Aidha,kuhusu fomula ya kikokotoo, Dkt. Nchemba alisema kuwa Kamati imeundwa na inahusisha watu mbalimbali na Wizara inayohusika na utumishi nayo inaendelea na zoezi kubwa linalohusisha masuala ya pensheni kwa ujumla wake.

Akizungumzia mafunzo kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina kabla ya kustaafu, alisema kuwa mafunzo yanaendelea kutolewa na yataboreshwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news