Shilingi milioni 12 za Halmashauri ya Momba zamponza Afisa Uvuvi Msaidizi

SONGWE-Mei 9, 2024 imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi namba 11973/2024 mbele ya Hakimu Mkazi, Mheshimiwa Tagha Komba wa Mahakama ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe.
Ilidaiwa mshtakiwa Mussa Ladislaus Twaha ambaye ni Afisa Uvuvi Msaidizi Kata ya Kamsamba mnamo Aprili 16, 2017 na Machi 6, 2019 akiwa na nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kinyume na Kifungu cha 31 cha PCCA Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.

Ni kwa kushindwa aidha kupeleka fedha kwa Mhasibu wa Halmashauri ya Momba au kuweka kwenye akaunti ya halmashauri hiyo kiasi cha shilingi 12,744,010.

Kosa hilo ni kinyume na agizo namba 37(2) na 50(5) ya Randama ya Fedha ya Serikali ya Mtaa ya mwaka 2009 na hivyo kujipatia maslahi binafsi.

Pia, mshtakiwa anakabiliwa na kosa la Ufujaji na Ubadhirifu, kinyume na kifungu cha 28(1) cha PCCA Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.

Anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa shilingi 12,744,010 mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba zilizofika kwenye himaya yake akiwa mtumishi wa umma.

Kesi inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU,Hilda Mtaki.

Mshtakiwa amekana makosa yake na yupo rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kesi itakuja Mahakamani Mei 16, 2024 kwa ajili ya hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news