Shilingi Trilioni 2.73 za Wizara ya Uchukuzi zinavyokwenda kugusa maisha ya Watanzania

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Uchukuzi, Mheshimiwa Prof. Makame Mabarawa leo Mei 6, 2024 amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni jijini Dodoma.
Amesema, katika kutekeleza mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Uchukuzi itatumia jumla ya shilingi trilioni 2.73.

Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 114.74 sawa na asilimia 4.2 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 2.61 sawa na asilimia 95.8 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango kwa mwaka 2024/25, wizara hiyo imepanga kutekeleza vipaumbele katika maeneo mbalimbali ikiwemo;

1. Utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea ambayo ni pamoja na:

i. Kuendeleza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR) katika maeneo yaliyobaki pamoja na ununuzi wa vitendea kazi (vicha na mabehewa) ambapo jumla ya Shilingi trilioni 1.511 zimetenga;

· Kufufua Reli ya MGR kipande cha Kilosa-Kidatu Kilomita 108 ambapo kimetengwa kiasi cha Shilingi bilioni 1.

ii. Ukarabati wa Reli iliyopo katika ya MGR Shilingi bilioni 312.03 zimetengwa;

iii. Kuendelea kuboresha na kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege tatu, vipuri, injini na kukarabati miundombinu wezeshi. Shilingi bilioni 324.5 zimetengwa;

iv. Ujenzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu, ambapo jumla ya Shilingi bilioni 190.00 zimetengwa;

a) Ujenzi wa Meli Ziwa Tanganyika

· Ujenzi wa meli mpya ya abiria 600 na mizigo tani 400 Shilingi bilioni 25.

· Ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 Shilingi bilioni 35.

· Kujenga kiwanda cha kujengea Meli chenye uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 5,000 Shilingi bilioni 30.

· Ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 Shilingi bilioni 20.

b) Ukarabati katika Ziwa Tanganyika

· Ukarabati wa meli ya MV Liemba Shilingi bilioni 5.

· Ukarabati wa meli ya mafuta ya MT Sangara Shilingi bilioni 1.5.

· Ukarabati wa meli ya MV Mwongozo Shilingi milioni 300.

v. Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya Ndege ambapo Shilingi bilioni 108.71 zimetenga;

· Ujenzi wa Kiwanja cha Arusha Shilingi bilioni 5.08.

· Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Lindi Shilingi bilioni 13.

· Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Moshi Shilingi bilioni 5.

· Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida Shilingi bilioni.

· Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Kiwanja cha Ndege cha Njombe kwa Daraja 4E. Shilingi milioni 692.

· Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimataifa cha Serengeti Shilingi bilioni 1.

· Usanifu wa kina wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya TAA Shilingi milioni 400.

· Ujenzi wa Kiwanja cha Mwanza Shilingi bilioni 15.

· Ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba Shilingi bilioni 3.48.

· Ujenzi wa Kiwanja cha Mtwara Shilingi bilioni 7.3.

· Ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro Shilingi bilioni 50.

· Uboreshaji na Upanuzi wa Jengo la Pili la Abiria JNIA Shilingi bilioni 6.08.

vi.Kukarabati na kuboresha Reli ya TAZARA ambapo Shilingi bilioni 13.69 zimetengwa;

vii. Kuendelea na ununuzi wa rada na vifaa vya hali ya hewa ambapo Shilingi bilioni 15.00 zimetengwa;

viii. Kuendelea kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na bandari nyingine zikiwemo zilizopo katika Maziwa Makuu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya TPA;

a. Ziwa Tanganyika

· Uboreshaji wa Bandari ya Kigoma kwa kujenga barabara za kiungo, Cargo Shed, Passenger Wharf and Lounge;

· kuendelea na ujenzi wa jengo la abiria (Passenger Lounge); na

· kuendelea na ujenzi wa Passenger Lounge na ukuta wa mizigo wa Lighter Quay katika Bandari ya Kibirizi na gati la Bandari ya Ujiji

b. Ziwa Nyasa

· Kuendelea na uboreshaji wa Bandari ya Ndumbi kwa kujenga barabara unganishi;

· Kuanza uboreshaji wa Bandari ya Mbambabay ili kuwezesha kuhudumia meli na shehena katika Bandari za Ziwa Nyasa.

c. Ziwa Victoria

· kuendelea na ujenzi wa Bandari za Bukoba, Kemondo Bay, Mwanza South na Mwanza North ili kuwezesha huduma kwa meli ya kisasa inayojengwa na Serikali kutia nanga.

ix.Kuendelea kuboresha vyuo vya mafunzo ya kisekta (NIT na DMI) ambapo jumla ya Shilingi bilioni 30.74 zimetengwa.

2. Kuanza uendeshaji wa treni ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam – Dodoma ambapo kwa sasa Wizara kupitia TRC inaendelea na majaribio ya miundombinu ya reli kwa ajili ya kuanza utoaji wa huduma hiyo rasmi ifikapo mwezi Julai, 2024;

3. Kuanza kutoa mafunzo ya urubani katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa lengo la kupunguza gharama za kusomesha marubani nje ya nchi; na

4. Kununua Boti ya Matibabu (Ambulance Boat) kwa ajili ya utafutaji na uokoaji katika Ziwa Victoria pale ajali zinapotokea ndani ya Ziwa hilo.

5. Kuendelea kutekeleza Mkakati wa upatikanaji wa Fedha za kigeni ambapo kwa mwaka 2024/25 pekee Wizara inatarajiwa kukusanya jumla ya Dola za Marekani milioni 762.41, sawa na takriban Shilingi trilioni 1.94.

6. Pamoja na masuala hayo ya kisekta, Wizara pia itaendelea kusimamia masuala ya watumishi, michezo na masuala mengine muhimu katika kuendeleza Sekta ya Uchukuzi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Mbali na hayo, Mheshimiwa Waziri Pro.Mbarawa amesema, wizara itaendelea kuchukua mikakati mbalimbali kuhakikisha inaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news