Spika Dkt.Tulia ateta na Balozi wa Marekani hapa nchini
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Michael Battle ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei, 2024.