Swahiba wa Mwalimu Nyerere apongeza uongozi wa Rais Dkt.Samia, atimiza miaka 99

DAR-Mwanasiasa mkongwe nchini, Alhadji Mustapha Songambele amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza vyema taifa.
Mzee Songambele ametoa pongezi hizo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Jumamosi, Mei 25, 2024.

Balozi Nchimbi alikwenda nyumbani kwa Mzee Songambele Mwananyamala jijini Dar es Salaam kumfikishia salam za pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia kwa kuadhimisha miaka 99 ya kuzaliwa kwake.
“Mfikishie salamu zangu mwambie anaongoza nchi vizuri sana…nchi imetulia…nchi iko baridi kabisa hata chama nacho kimetulia mambo yanakwenda vizuri kabisa,” amesema Mzee Songambele.

Ameongeza kuwa, iwapo mambo yangekuwa hayaendi vizuri, basi pamoja na umri wake mkubwa, angeenda makao makuu ya chama kusema.
Kwa upande wake, Balozi Nchimbi amesema, Mzee Songambele alifanya kazi kubwa ya kujenga Chama na Serikali tangu enzi za TANU na baadae CCM.

Mzee Songambele alizaliwa mwaka Mei 25,1925, mkoani Ruvuma kabla ya kuhamia Magomeni, jijini Dar es Salaam, ambapo walikuwa miongoni kwa watu waliompokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere jijini humo.

Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwalimu Nyerere na ndiye aliyemtafutia kiwanja Magomeni Mikumi ambako kuna nyumba ya Mwalimu, hivi sasa ikiwa ni Makumbusho ya Taifa.

Aliwahi kushika nafasi kadhaa ndani ya chama na Serikali, ikiwa ni pamoja na ukuu wa mkoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news