Tanzania inatambua michezo ya majeshi ni nguvu kubwa ya kidiplomasia-Dkt.Mpango

DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema, Tanzania inatambua michezo ya majeshi ni nguvu kubwa ya kidiplomasia inayovuka mipaka na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Balozi.Dkt. Stergomena Tax wakati alipowasili Johari Rotana Jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) tarehe 14 Mei 2024. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) uliofanyika Johari Rotana Jijini Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali wa Majeshi Duniani wakiimba Wimbo wa Taifa la Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) uliofanyika Johari Rotana Jijini Dar es salaam tarehe 14 Mei 2024.

Amesema kwa uzoefu wa Tanzania katika kushiriki misheni mbalimbali za ulinzi wa amani inatambua michezo ya majeshi kama njia ya kuchochea amani, maelewano na kuheshimiana.

Aidha amesisitiza Baraza hilo kuhimiza amani duniani na kufanya jambo hilo kuwa ajenda ya michezo ya majeshi kimataifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akivishwa Medali na Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani Kanali Nilton Rolim kuwa Kamanda wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliyofanyika Johari Rotana jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei 2024.

Pia Makamu wa Rais ametoa wito wa Michezo ya Majeshi kutumika katika kupambana na Uharibifu wa Mazingira pamoja na kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza duniani kote. Amesema michezo hiyo inapaswa kutumika katika kuimarisha utimamu wa mwili na lishe bora kwa Majeshi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa michezo katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akivishwa Medali na Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani Kanali Nilton Rolim kuwa Kamanda wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo uliyofanyika Johari Rotana Jijini Dar es salaam tarehe 14 Mei 2024.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani kuwa mstari wa mbele katika kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli duniani kote. Amesihi Baraza hilo kuweka mipango thabiti katika kukuza vipaji vya wanajeshi vijana pamoja na raia kwa kuanzisha vituo vya michezo.

Pia amesema ni muhimu kuimarisha usawa wa kijinsia katika michezo ya baraza hilo kwa kuhamasisha na kuhakikisha ushiriki wa wanawake unaongezeka na michango yao inathaminiwa.
Makamu wa Rais amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani katika kuandaa michuano hiyo hapo baadae.

Amesema ni muhimu michuano hiyo kuandaliwa na kufanyika katika nchi wanachama na pale kunapokuwa na changamoto ya miundombinu mataifa yanapaswa kushirikiana katika kuandaa michuano hiyo kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya na Uganda wanavyoshirikiana kuandaa michuano ya Afrika (AFCON).

Mkutano huo umekutanisha washiriki 320 kutoka mataifa ya Ulaya, Amerika, Asia na Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news