Tanzania itaendelea kushirikiana na UNICEF-Waziri Mkuu

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Elke Wisch, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Waziri Mkuu amemuahidi Bi. Wisch kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kulipa ushirikiano Shirika hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, maji na elimu.
Kwa upande wake, Bi. Wisch ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mipango katika kuboresha sekta ya elimu, mpango wa kukabiliana na maafa pamoja na kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha, Bi. Wisch ameahidi shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuandaa na kutekeleza mpango kazi wa kukabiliana na maafa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news