Tanzania na Msumbiji zaangazia fursa Sekta ya Biashara

MAPUTO-Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mhe. Silvino Augusto José Moreno, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye ofisi ya wizara hiyo jijini Maputo.
Hayo ni mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 22,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo.
Katika mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ili kufanikisha ushirikiano katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji.
Vilevile, viongozi hao wamekubaliana kutafuta mbinu na mikakati mahsusi ya kuongeza kiwango cha biashara baina nchi hizi ili kiende sambamba na uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia baina ya nchi hizi.
Moja ya maeneo yaliyopendekezwa ni kuanzisha Jukwaa la Pamoja la Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wadau wengine muhimu ili kubadilishana uzoefu, kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na kubaini namna ya kunufaika nazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news