Tanzania yasaini Paris Declaration

PARIS- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufaransa zimesaini Tamko la Paris (Paris Declaration) katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo baina ya nchi hizo mbili.
Tamko hilo limesainiwa Mei 14, 2024 jijini Paris Ufaransa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou.
Maeneo ya ushirikiano yaliyosainiwa ni pamoja na Nishati na mabadiliko ya tabianchi, usafirishaji na maendeleo ya miundombinu, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.
Hafla ya utiaji saini imeshuhudiwa na Mabalozi wanaowakilisha katika hizo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Jabir Mwadini, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Nabil Hajlaoui, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda na Maafisa wengine Waandamizi walioambatana na Viongozi hao wawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news