DAR-Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilosa na Waziri wa Fedha na Uchumi,Mheshimiwa Mustafa Haidi Mkulo amefariki usiku wa kuamka leo wakati akiendelea na matibabu Hospiali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkewe Bi.Julie Mkulo ambapo amesema, kifo cha mume wake kimetokea leo Mei 4,2024.
Aidha,shughuli zote za mazishi zitakuwa nyumbani Mikocheni leo na maziko yatakuwa Mei 5,2024 huko Kilosa mkoani Morogoro.