DAR-Teknolojia mbadala ya kuimarisha mtandao wa barabara ikiwemo ujenzi wa madaraja imara na madhubuti itaendelea kutumiwa nchini na Wakala wa Barabara za Vijijini na Vijijini (TARURA).

“TARURA wanaonesha utaalamu, wanafanya ikiwemo ujenzi wa ‘structure’ mbalimbali za kupitishia maji, wanajenga kwa mawe teknolojia ambayo inapunguza gharama,” amesema.
Akizungumza namna Serikali ilivyojipanga kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mvua zilizoanza kunyesha tangu Oktoba, 2023 na zinazoendelea hadi sasa, Naibu Katibu Mkuu Mativila amebainisha kwamba bado kuna sehemu nyingi mvua zinaendelea kunyesha, miundombinu mingi imeharibika, mvua zilizokuja hazikuwa za kawaida kama miaka mingine.
Hata hivyo amesema,wameshafanya tathimini na zinahitaji kiasi cha shilingi bilioni 2 kurejeresha miundombinu iliyoharibiwa na mvua na Serikali ipo tayari kutoa fedha hizo
Naye msimamizi wa Teknolojia Mbadala TARURA Makao Makuu,Mhandisi Mshauri Pharels Ngeleja amesema,tayari wamejenga madaraja 256 kwa teknolojia ya mawe yaliyogharimu shilingi bilioni 13.

“Tumejenga barabara ya Sawala kilomita 13 mkoani Iringa, Chamwino - Dodoma pia tunaendelea na hizi teknolojia, Dodoma kuna barabara inaitwa daraja dogo tumekamilisha.Miradi hii ipo maeneo mbalimbali ambapo tunaendelea,” amesema Mhandisi Ngereja.

TARURA imeweza kujenga barabara kwa kutumia teknolojia ya Ecoroad, Ecozyme na Polymer katika barabara ya Chamwino Km. 7,Itilima Km. 5, Sawala-Mkonge Km. 10 na Daraja dogo -Dodoma Km.1.