DAR-Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent na watendaji wake wamekutana katika kikao na maafisa watendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom nchini ili kujadili mashirikiano baina ya mamlaka na kampuni hiyo ya simu.
Majadiliano hayo yamelenga kufanya tathmini ya ushiriki wao katika utekelezaji wa mpango wa ruzuku kwa msimu wa kilimo wa 2023/2024 tunapoelekea mwishoni kwa msimu wa kilimo.
Kampuni ya Vodacom imeonesha utayari wake kuendelea kushirikiana na mamlaka katika nyaja ya mafunzo ya matumizi ya vishikwambi kwa maafisa ugani wakati wa zoezi la usajili wa wakulima na mafunzo ya utoaji huduma kwa wateja wa mbolea kwa msimu ujao wa kilimo.