Balozi Yakubu,TIC kushirikiana kuvutia wawekezaji Comoro

DAR-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro, Mhe.Said Yakubu amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Gilead Teri leo Mei 8, 2024 katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao Mhe. Balozi na Bw. Teri wamejadili namna ya kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro ambako Balozi huyo anaenda kuiwakilisha Tanzania.
Kupitia ushirikiano huo TIC imeahidi kupeleka ujumbe wa kwanza wa wawekezaji angalau 20 mwishoni mwa mwezi Juni, 2024 na itashirikiana na Taasisi za sekta binafsi kuandaa ziara za wawekezaji kila mwezi kati ya Julai na Disemba 2024 kuangalia sekta mbalimbali ikiweka kipaumbele katika sekta ya uchukuzi, fedha, afya, utalii na ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news