TIRA yatoa somo la kujisajili kwa wamiliki wa gereji

DAR-Kamishna wa Bima, Dkt.Baghayo Saqware amewataka wamiliki wa gereji za kutengeneza magari, kujisajili katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ili kuepusha changamoto ikiwemo udanganyifu, ucheleweshwaji wa malipo na huduma mbovu kwa wateja wao ambapo TIRA inawajibika kusimamia haki za pande zote mbili.
Dkt.Baghayo ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa semina ilitolewa kwa wanaotoa huduma za bima nchini, zikiwemo kampuni za Bima na Umoja wa Watengenezaji na Warekebishaji wa vyombo vya moto ili wafuate mwongozo sahihi wa utoaji wa huduma hizo uliotolewa na TIRA.
Pia, Kamishna amekubali ombi la kuwa Mlezi wa Chama cha Wamiliki wa Gereji na kuwataka kutanua wigo wa wanachama kwa kuongeza wanachama hasa mafundi kujiunga katika chama hicho ili na wao wawe na uelewa wa pamoja kuhusu bima.

Naye Mwenyekiti wa muda wa Chama Cha Wamiliki wa Gereji, Hendry Lema, ameiomba TIRA kuweka mazingira rafiki ya usajili na kutoa elimu ili kuwafikia watu wengi zaidi, huku wakipendekeza kuwepo adhabu kwa wamiliki wa gereji ambao watashindwa kufuata miongozo na pia kuwe na fursa sawa za ufanyiaji kazi wa marekebisho au matengenezo ya magari yaliyokatiwa bima.

Meneja Madai kutoka Kampuni ya Bima ya Britam, Neema Mathayo amesema mwongozo huo unatasaidia kumaliza udanganyifu ambao umekuwa ukijitokeza mara Kwa mara katika huduma hizo, huku mwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Lugano Mwasomola akisema mwongozo huo utakuwa na msaada mkubwa.
Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki, Zacharia Muyengi amesema mafunzo hayo ni mwendelezo, ambapo pia washiriki wanafundishwa mifumo ya mamlaka na mfumo wa kujisajili, utaratibu wa nyaraka zinazohitajika wakati wa usajili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news