ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwaombea dua viongozi ili watimize majukumu yao na kutekeleza ahadi walizoahidi.

Pia Rais Dkt.Mwinyi amewatembelea Wazee akiwemo Mbunge wa zamani Jimbo la Amani , Mzee Hassan Rajab nyumbani kwake Kisauni na Mjumbe wa Baraza la Wazee CCM Kisiwandui, Bi Maryam Hengwa nyumbani kwake kwa Mchina Mkoa wa Mjini Magharibi.