Ukarabati MV.Magogoni kukamilika Desemba 2024

DODOMA-Ukarabati wa Kivuko cha MV. Magogoni unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba, 2024 na kurejeshwa nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya Bungeni jijini Dodoma leo Mei 30, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni,Dkt. Faustine Ndungulile.

Mheshimiwa Dkt.Ndungulile aliuliza ni lini matengenezo ya Pantoni ya MV. Magogoni iliyopo nje ya nchi yatakamilika na kurejeshwa nchini ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Itaumbukwa kuwa,mwezi Februari 2023 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ilisaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5.Lengo la ukarabati huo wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini.

Pia,kuharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news