VIDEO:Kuelekea uzinduzi wa Kituo cha Umeme Ifakara, wananchi wafunguka

MOROGORO-Wakazi wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilika na kuanza kutumika kwa Kituo cha Kupoza umeme cha Ifakara.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamesema kuwa, zamani walikuwa na changamoto kubwa ya kukatika katika kwa umeme katika eneo hilo hali iliyoathiri shughuli zao za kiuchumi na upatikanaji wa huduma muhimu.
Kituo hicho cha Kupoza Umeme cha Ifakara kimejengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa Ufadhili wa Umoja wa Ulaya ambapo mpaka kukamilika kwake, jumla ya fedha za Kitanzania shilingi bilioni 25 zimetumika.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Christine Brau wanarajiwa kuzindua rasmi Kituo hicho, Ijumaa, tarehe 31 Mei, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news