Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewatakia wanafunzi wote wa Kidato cha Sita na Walimu taraji kila la heri katika mitihani yao ambayo inaendelea nchini.
Mitihani ya Kidato cha Sita (ACSEE) na Ualimu ngazi ya cheti na Stashahada imeanza rasmi Mei 6,2024 kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wa kidato cha sita utakamilika Mei 24,2024 wakati wa Ualimu utakamilika Mei 20,2024.
Aidha, mtihani wa kidato cha sita utafanyika katika shule za sekondari 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258 na vituo vya ualimu 99.