TANGA-Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amekabidhi majiko banifu pamoja na majiko ya gesi kwa wakazi wa Kijiji cha Msomera, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga jana Mei 17 ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Serikali za kuhakikisha ifikapo 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.
Katika hafla hiyo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umetoa majiko banifu 1500 yenye gharama ya Shilingi Milioni 82.5 ikiwa ni muendelezo wake katika kufanikisha azma hiyo ya Serikali yenye lengo la kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Tags
Habari
Majiko Banifu
Majiko ya Gesi
REA Tanzania
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Wizara ya Nishati Tanzania