Vijana wa Kitanzania waibuka kidedea TEHAMA China, Waziri Nape awapa kongole

DAR-Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, amewapongeza vijana watatu wa Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Ndaki ya ICT (CoICT) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya TEHAMA duniani ya Huawei yaliyofanyika Mei 23 hadi 26, 2024 Shenzhen, China.
Vijana hao ni Dickson Mram, Matimu Mahimbo na James Amos ambao wana ujuzi katika uhandisi wa kompyuta, IT na mawasiliano ya simu, waliambatana na Mhadhiri msaidizi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Mhandisi Jumanne Ally walishiriki katika mashindano hayo yaliyowashindanisha wanafunzi zaidi ya 470 kutoka nchi 49 duniani.

Waziri Nape amesema kuwa, ushindi huu unaonyesha uwezo uliopo miongoni mwa vijana wetu wa kitanzania katika fani muhimu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.Vijana hao watarudi Tanzania tarehe 28 Mei, 2024 na wanawatarajiwa kupokelewa kwa shangwe na kupongezwa kwa kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine wa kitanzania.

Waziri Nape ameuzungumzia ushindi huo kuwa mwanzo mzuri wa kujenga taifa lenye ubunifu katika fani za TEHAMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news