Vishoka wanaoshikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi kuchukuliwa hatua

DODOMA-Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema, Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kujihusisha na mchezo mchafu wa kushikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi.
Bashungwa ameyasema hayo Mei 19,2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Amesema, changamoto kubwa ni uwepo wa vishoka wanaoshikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi na kutoza fedha nyingi.

Bashungwa amesema, Wizara ya Ujenzi inaendelea na mazungumzo na Wizara ya Madini kuhusu upatikanaji wa malighafi ya ujenzi ikiwemo changarawe, mchanga na kokoto.

“Mazungumzo hayo yanalenga kupata namna bora ya kutatua changamoto kubwa ya upatikanaji wa malighafi hizo.

“Dhamira ya wizara ni kuwa kwa kadri inavyowezekana maeneo hayo yamilikishwe TANROADS ili kuwezesha miradi mingi ya barabara kutekelezwa kwa wakati, na kupunguza gharama za ujenzi.”

Amesema, upatikanaji wa malighafi ya ujenzi kwa gharama nafuu itawezekana iwapo TANROADS itakuwa na maeneo ya kuchimba madini ya ujenzi na kuondokana na hali ya sasa ya vishoka wanaopandisha gharama za ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news