Watendaji jela kwa kuomba hongo shilingi milioni 3 ili mwanakijiji aishi kwa amani

TABORA-Aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Imagi Kata ya Nh'wande, Richard Maganga Mpagama na Laurent Isaya Sendu, Mtendaji wa Kata ya Nh'wande wilayani Kaliua mkoani Tabora wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 3.
Hukumu hiyo imetolewa Mei 24, 2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Mheshimiwa Felix Ginene.

Kesi hiyo ilikuwa ya Jinai Na.71/2023 ambayo ni Jamhuri dhidi ya Richard Maganga Mpagama na Laurent Isaya Sendu.

Aidha,kesi iliongozwa na waendesha Mashtaka wa Serikali David Bakari pamoja na Kajivo Aidan.

Wawili hao wametiwa hatiani kwa kosa la kuomba na kupokea hongo ya shilingi 3,000,000 kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na (2) cha PCCA (Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022).

Ilielezwa kwamba Mei 21,2023 watuhumiwa
Richard Maganga Mpagama akiwa ni Mtendaji wa Kijiji cha Imagi, Kata ya Nh'wande na Laurent Isaya Sendu, Mtendaji wa Kata ya Nh'wande wilayani Kaliua mkoani Tabora, waliomba rushwa ya shilingi 3,000,000 kutoka kwa mwananchi mkazi wa Kijiji cha Imagi, Kata ya Nh'wande wilayani Kaliua, Bw. Ndilana Budeba.

Ni ili wamwachie huru na aishi kwa amani katika kijiji hicho kwa kosa alilounganishwa lililomhusu mkwe wake (mume wa binti yake) kuhusika na wizi wa kutumia silaha.

Washtakiwa wametiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. 1,000,000 kila mmoja na kuamriwa kumrejeshea Ndilana Budeba kiasi cha shilingi 2,300,000.

Hiyo, ikiwa ni sehemu ya fedha iliyobaki baada kumrejeshea kiasi cha shilingi 700,000 wakati uchunguzi ukiwa unaendelea.

Hata hivyo,washtakiwa wameshindwa kulipa faini na hivyo wamepelekwa gerezani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news