ARUSHA-Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza Kikao cha Ujumbe wa Tanzania, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCTIFI) unaofanyika leo tarehe 31 Mei, 2024, ambapo masuala kadhaa yanayohusu maendeleo ya sekta ya biashara katika nchi wanachama hususan masuala ya kodi, yatajadiliwa.
Kwa upande wa Tanzania, Mkutano huo umewashirikisha pia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Shariff Ali Shariff, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigae, Waziri wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara za Kisekta.