Waziri Makamba aagana na Balozi wa Italia nchini

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba ameagana na Balozi wa Italia nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.Akizungumza katika kikao hicho Waziri Makamba amemtakia kila la heri Balozi Lambardi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Italia.
“Uliukuta uhusiano wa Tanzania na Italia ukiwa katika hali nzuri lakini kwa nguvu, jitihada na weledi wako umeufanya uhusiano wetu kuwa katika kiwango cha juu kabisa, tunakupongeza na kukushukuru sana,” alisema Waziri Makamba.

Naye Balozi Lambardi ameishukuru Idara ya Amerika na Ulaya - Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa iliyompatia wakati wote ambao amekuwa kitekeleza majukumu yake nchini.

“Mhe. Waziri niwashukuru sana Wizara na hasa Idara ya Ulaya na Amerika kwa kushirikiana nami na kufanya utendaji wangu kukamilika bila kukwama, asanteni sana,” alisema Balozi Lambardi.
Amesema,ana amani kuwa anaondoka nchini huku akiuacha mpango wa Matei ukiwa katika hatua nzuri ya utekelezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news