Waziri Mhagama ashiriki Mkutano wa Kujadili hali na athari za mvua za El-Nino ukanda wa SADC

DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameshiriki katika Mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El Nino katika Ukanda wa SADC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na wajumbe kutoka Wizara zinazohusika na Masuala ya Kilimo, Maji, Nishati na Uratibu wa Udhibiti wa Maafa wa nchini Tanzania wakati wa Mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El Nino katika Ukanda wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao Jijini Dodoma.
Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya Mtandao (Zoom meeting) tarehe 14 Mei, 2024 Jijini Dodoma ukihusisha Wizara za Kisekta zinazohusika na Masuala ya Kilimo, Maji, Nishati na Uratibu wa udhibiti wa Maafa ni maandalizi ya Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Kuhusu Hali ya Mvua za El nino utakaofanyika kwa njia ya Mtandao Mei 20, 2024.




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news