Waziri Mkuu akagua shamba la mkulima wa kakao Kyela

MBEYA-Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa leo Mei 12, 2024 ametembelea shamba la Mkulima zao la Kakao Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela leo Mei 12, 2024.
Akizungumza baada ya kulitembelea Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakulima wa zao hilo wajisajili na watambue idadi ya miche waliyonayo na ukubwa wa mashamba yao ili wakati Serikali ikitoa ruzuku kila mkulima anufaike na kuiwezesha Serikali kujua ni tani kiasi gani itazalishwa.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakulima na viongozi wa AMCOS wasimamie ubora zao la Kakao na kuzitumia fedha wanazopata baada ya mauzo kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news