Waziri Mkuu awataka wakandarasi miradi ya umwagiliaji kuzingatia ubora

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakandarasi wazawa waliopewa dhamana ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliji kuhakikisha waaitekelza kwa weledi na ubora wa hali ya juu.
Majaliwa ameyasema hayo jana katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali, iliyofanyika jijini Dodoma.

"Ndugu washiriki nimefurahishwa kuona kuwa asilimia 82 ya wanaokwenda kujenga miradi hii ni wataalamu na hizi ni fursa za ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa ya kuongeza ujuzi kupitia miradi hii, vilevile inakwenda kuongeza kipato kwa Watanzania.

"Nitoke rai kwa wakandarasi wazawa, kwanza mbadilike, mnathaani kubwa mmepewa ya kutekeleza miradi na hili ndicho kilio kikubwa cha private sector (sekta binafsi) leo mmeona serikali imeendelea kutekeleza kwa kuwapa miradi.

"Mjipange vizuri tumieni fursa hii kuihakikishia serikali kwamba mnaweza, lakini nyie mna dhamira zenu kufungua kampuni za ukenzi, mna hiyo dhamira simamieni dhamira zenu. Sisi tunakutegemeeni nyie kufua milango ya ajira."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news