Waziri Mkuu azindua Kituo Atamizi cha Ufugaji wilayani Kongwa

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 13, 2024 amezindua na kushuhudia makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana kilichopo Kongwa mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya makabidhiano ya kituo hicho, ambacho kinathamani ya shilingi bilioni 1.63 ikijumuisha uwekezaji wa vifaa na mindombinu, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza uwekezaji utunzwe ili taifa liweze kunufaika kupitia uwezeshwaji wa vijana.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwapatia vijana ujuzi kwa vitendo ikiwemo elimu ya ujenzi wa mabanda, ulishaji, matibabu na usimamizi wa mbuzi lakini pia kutoa mafunzo ya biashara ili vijana waweze kuwa wajasiriamali na kuendeleza biashara ya unenepeshaji mbuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news