Waziri Ndejembi apata ushuhuda wa mstaafu anayepokea pensheni PSSSF

ARUSHA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, amepata ushuhuda wa mstaafu anayepokea Mafao yake kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Mhe. Ndejembi amepata ushuhuda huo kutoka kwa Bw.Thomas Shuma, ambaye ni mstaafu na kwa sasa anapokea mafao yake PSSSF, wakati alipomkuta kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika viwanja vya general tyre jijini Arusha Aprili 29, 2024.

Bw.Shuma alikuwa akipatiwa huduma ya kujiunga na PSSSF Kiganjani App, inayomuwezesha mwanachama kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wastaafu kujihakiki kupitia simu janja.
Mhe. Ndejembi alimuuliza Bw. Shuma, huduma unaipata vizuri? Na kujibiwa ninaipata vizuri kabisa, kisha Mhe. Waziri akamuuliza tena, vipi kuhusu malipo ya pensheni yako, mzee Shuma akajibu pensheni yangu naipata kwa wakati

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news