Waziri Pembe aitaka Bodi ya Ushauri ya Watoto Taifa kuwa na umoja

ZANZIBAR-Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar,Mheshimiwa Riziki Pembe Juma ameitaka Bodi ya Ushauri ya Watoto Taifa kuwa na umoja moja katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Ameyasema hayo jana wakati alipokutana na bodi hiyo Ofisini kwake Kinazini Mjini Unguja.

Amesema, kwa sasa inaonekana watoto wa kiume kuharibiwa kwa kasi. Hivyo Mhe. Riziki amewataka wajumbe wa bodi hiyo kuunganisha nguvu ya pamoja katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Mhe. Riziki amefahamishwa kwamba, wizara anayoisimamia imeundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii nchini, ikiwemo masuala yanayowahusu watoto, hivyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha changamoto zinazowakabili watoto wanaziwasilisha katika wizara hiyo ili kuweza kupatiwa ufumbuzi.
Aidha,amewataka kuhakikisha wanabadilisha mitazamo ya baadhi ya watoto wanokataa kushiriki katika vikao au wito wowote kwa kuona kwamba hakuna malipo ya fedha au zawadi, kwani hali hiyo inaweza kutoa fursa kwa watu wabaya kutumia mwanya huo na kuwaharibu.

Amewahakikishia kuwa changamoto zinazowakabili katika bodi kupitia wilaya zao, wizara itajitahidi kuzifanyia kazi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuona mafanikio yanapatikana juu ya kunzishwa mabaraza hayo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Taifa, ndugu Tatu Khamis Ramadhan ameelezea kufurahishwa kwake kwani ni mara ya kwanza bodi hiyo kukutana na waziri wao, na kuelezea changamoto zinazowakabili ikiwemo ndoa za utotoni, baadhi ya vijiji kutofuatwa ipasavyo Sheria ya Mtoto Na.6 ya mwaka 2011 ambayo inaeleza haki za mtoto.
Hata hivyo, ameiomba wizara kuwapatia vyeti maalumu wajumbe au viongozi waliomaliza kutumikia mabaraza ya watoto ili iwe ni uthibitisho kwao kwamba wamejitolea kutumikia taifa lao.

Pia wameomba kufanya uwezekano wa kuwekwa vituo vya one stop center katika hospitali mbalimbali ili iwe rahisi kupatiwa huduma za matibabu kwa waliopata tatizo la udhalilishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news