Waziri Prof.Mkenda ashiriki Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Elimu Jumuiya ya Madola

LONDON-Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ameshiriki Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Elimu wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Marlborougj House jijini London, Uingereza kuanzia tarehe 16 hadi 17 Mei 2024.
Mkutano huo unakutanisha Mawaziri wa Elimu, Taasisi za Jumuiya ya Madola, Mashirika ya Kimataifa kama UNESCO na Benki ya Dunia pamoja na wadau wengine wa elimu.

Lengo ni kujadili namna nchi wanachama zinavyoweza kuweka mikakati stahimilivu itayoweza kuifanya elimu iwe endelevu katika kipindi cha majanga kama UVIKO-19.

Pia, kuongeza fursa na usawa katika kuelimisha watu katika jamii na kutumia teknolojia mpya kama vile akili bandi na teknolojia za kidijitali katika kurahisisha utoaji na upatikanaji wa elimu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Kutokana na JYM kuwa na uwakilishi wa nchi kubwa na visiwa vidogo, Sekretarieti ya Jumuiya hiyo inatumika kama jukwaa la kubadilishana uzoefu, kupeana maarifa na misaada ya kiteknolojia na kiufundi katika kutimiza azma hiyo.
Pichani ni Mhe. Waziri Mkenda akiwa pamoja na Mhe. Patricia Scotland, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Pamoja na masuala mengine, Mkutano huo unatoa fursa kwa Mawaziri kujadili mchango wa ubunifu (innovation) katika kuimarisha sekta ya elimu.

Kipaumbele cha Serikali katika Mkutano huo ni kuona namna Tanzania inavyoweza kunufaika na ushirikiano na nchi wanachama wa Junuiya hiyo katika kuimarisha utoaji wa elimu ya ufundi na ujuzi mbalimbali utakaosaidia kupanua soko la ajira kwa vijana sambamba na mfumo rasmi wa elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news