Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni chachu ya maendeleo sekta za uzalishaji-DC Kaji

TANGA-Mkuu wa Wilaya ya Tanga mkoani Tanga, Mhe. James Kaji amesema, Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu italeta chachu ya maendeleo ya viwanda na uchumi kwa Mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Mhe. Kaji amesema hayo Mei 26, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal ambapo amesisitiza Wanatanga kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo teknolojia na ubunifu.

"Maadhimisho haya yanawapa wananchi nafasi ya kujifunza masuala ya Ujuzi na Ubunifu kuwezesha vijana wa Kitanzania kushiriki katika sekta mbalimbali za uzalishaji na hivyo kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,"amesema Kaji.

Aidha, ameishukuru Serikali chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali ya Elimu nchini na kwamba maadhimisho haya ni fursa ya pekee kwa Wakazi wa Tanga kushiriki kutoa hamasa masuala ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news