Zambia wafika kujifunza Tanzania kuhusu miradi

DODOMA-Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Zainabu Katimba amekutana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ya Zambia na kubadilishana uzoefu juu ya miradi inayotekelezwa kupitia mfuko wa jimbo na mapato ya ndani ya mamlaka za Serikali za mitaa. Mhe. Katimba amekutana na wajumbe wa kamati hiyo leo Mei 16, 2024 jijini Dodoma kabla ya kufanya ziara yao ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia fedha za mfuko wa jimbo na mapato ya ndani.
Akifafanua kuhusu Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, Mhe. Katimba amesema, mfuko huo ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge ya 2009 kwa lengo la kuhakikisha miradi ambayo ni vipaumbele vya wananchi katika jimbo husika na ambayo havikupata fedha katika bajeti inapata fedha za utekelezaji.
Amesema,ni fedha za jimbo kwa ajili ya majimbo ya uchaguzi ambayo yameanzishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia Katiba.

Aidha, amesema katika kuwanufaisha wananchi na miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, Mfuko unawapa fursa watu binafsi wanaofanya kazi katika ngazi ya chini kupitia wabunge wao kushiriki kikamilifu katika kufanya uchaguzi wa matumizi ambayo huongeza ustawi wao kulingana na mahitaji na mapendeleo yao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ya Zambia, Mhe. Darios Mulunda ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na kuleta maendeleo kwa wananchi,

Amesema,utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupiti mfuko wa jimbo na mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kunasaidia kuharakisha maendeleo kwa wananchi na kuongeza imani na Serikali yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news