Afisa Mtendaji wa Kata jela miaka mitatu kwa kuomba na kupokea rushwa

MARA-Alloyce James Emanuel ambaye ni Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Chitengule Wilaya ya Bunda mkoani Mara amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa.
Hukumu hiyo imetolewa Juni 11, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda kupitia kesi ya Jinai Na.01/2023 mbele ya Mhe. Mulokozi Kamuntu, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo.

Katika shauri hilo lililoendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU,Bw. William Lyamboko, mshtakiwa Bw. Alloyce James Emanuel ambaye ni Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Chitengule Wilaya ya Bunda, alishtakiwa kwa kosa la kuomba hongo ya shilingi 130,000.

Hilo likiwa ni kosa chini ya kifungu cha 15(1)(a) na (2 ) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Bw.Lyamboko alieleza kuwa mnamo Oktoba 14, 2022 mshtakiwa aliomba hongo hiyo kutoka kwa Simon Kadilahna Shija ili aweze kuwaachia ng’ombe wake baada ya kuwakamata wakifanya uharibifu wa mazao katika maeneo ya mashamba ya watu.

Mahakama imemhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh. 500,000 kwa kila kosa,hivyo kwa makosa yote mawili aliyoshitakiwa nayo alipaswa kulipa sh. 1,000,000.

Mshtakiwa amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa faini hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news