SIMIYU-Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihangosi leo Juni 19,2024 amefunga mafunzo ya wiki sita ya ulinzi shirikishi kwa askari wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,Mheshimiwa Simon Simalenga kwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kufanyika kwa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Mkaguzi kata wa Kata ya Gambosi, Mkaguzi wa Polisi Francis Msuku.