BAKWATA yatangaza Juni 17,2024 ni Sikukuu ya Eid el Adh’haa

DAR-Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema, Sikukuu ya Eid el Adh’haa itakuwa Jumatatu ya Juni 17 na sala yake itaswaliwa katika msikiti wa Mohamed VI uliopo makao makuu ya baraza hilo Kinondoni.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 8, 2024 na Katibu Mkuu wa BAKWATA Taifa, Alhaji Nuhu Mruma.

Amesema,sala ya Eid itaanza saa moja asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika pia katika msikiti huo.

“Kwa niaba ya BAKWATA, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir anawatakia maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” amesema Alhaj Mruma katika taarifa hiyo.

Eid El Adh’haa ni sikukuu inayoadhimishwa baada ya waumini wa Kiislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za dini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news