Balozi Dkt.Nchimbi aongoza waombolezaji maziko ya Tixon Nzunda mkoani Songwe

SONGWE-Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi ameongoza maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi na wananchi kutoka maeneo mnalimbali nchini, walioshiriki maziko ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda.
Maziko hayo yamefanyika Juni 22,2024 huko Msinde katika Kata ya Mpemba, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Marehemu Nzunda ambaye hadi mauti unamkuta kwa ajali ya gari Juni 18, 2024, akiwa ziara ya kikazi wilayani Hai, alikuwa mtumishi mwandamizi wa Serikali, akiwa amewahi kutumikia nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, ikiwemo kuwa katibu mkuu wa wizara mbalimbali, baada ya kupanda ngazi za utumishi wa umma kutokea kuwa Ofisa wa Serikali ngazi ya wilaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news