Balozi Dkt.Nchimbi atoa heshima za mwisho kwa marehemu Tixon Nzunda

DAR-Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amejumuika pamoja na waombolezaji wengine, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Tixon Nzunda, shughuli iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Goba jijini Dar Es Salaam.
Balozi Dkt.Nchimbi, ambaye alisoma pamoja na marehemu Nzunda Chuo Kikuu Mzumbe, pia aliwapatia pole familia ya marehemu kwa msiba huo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.

Mwili wa marehemu Nzunda, ambaye alifariki kwa ajali ya gari Juni 18, 2024 huko wilayani Hai, unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao, mkoani Songwe, Juni 22, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news