
Dkt.Nchimbi amewasili Arusha, tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwenye mikoa mitano, ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Hamid Abdallah.