Balozi saba zaunganishwa na Mfumo wa Uhasibu Serikalini (MUSE)

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Fedha katika mwaka wa fedha 2023/2024 imefanikiwa kuziunganisha ofisi saba za balozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mfumo wa Uhasibu Serikalini (MUSE).
Hayo yamebainishwa leo Juni 4, 2024 na Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.

Waziri Dkt.Nchemba amesema, kwa mwaka 2023/24, wizara ilipanga kuboresho Mfumo wa Uhasibu Serikalini (MUSE), kuboresha Mfumo wa Usimamizi wa Bajeti (CBMS),

Pia, kuunganisha mfumo wa MUSE na mifumo mingine ya usimamizi wa fedha za umma ikiwemo kuboresha Mfumo wa Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMIS) na kuunganisha balozi 10 za Tanzania katika mfumo wa MUSE.

Vile vile, kuunganisha taasisi mpya na mfumo wa MUSE na kuzijengea uwezo taasisi katika matumizi ya mifumo ya usimamizi wa fedha za umma.

"Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2024, wizara imefanikiwa kuboresha mfumo wa CBMS ili kuongeza ufanisi katika udhibiti wa mipango na bajeti ya Serikali.

"Na kuunganisha mfumo wa MUSE katika balozi saba za Tanzania katika nchi ya Ufaransa, Austria, Ujerumani, Uturuki, Uingereza, China na Uswisi na kuboresha moduli tano za mfumo wa GAMIS."

Mbali na hayo amesema, wizara imetoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa GAMIS kwa taasisi za umma 269.

Kazi nyingine zilizotekelezwa ni kuwezesha taasisi za umma 477 kuandaa taarifa za hesabu za fedha kwa kutumia mfumo wa MUSE, kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo wa MUSE katika balozi 17 za Tanzania na kuunganisha mfumo wa MUSE kwenye taasisi za umma 15.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news